Watu wengi sana wanafanya matangazo ya kulipia Facebook na Instaram lakini


 

Facebook ads

Watu wengi sana wanafanya matangazo ya kulipia Facebook na Instaram lakini.Ni wachache tu kwenye hao wengi wanaopata matokeo mazuri.

Wakati wengi sana wanaishia kupoteza hela nyingi na kuwa na akaunti zenye madeni makubwa.Ipo sababu kwanini wachache wanapata matokeo mazuri.

Na sababu hiyo ni kwamba Wachache wanaopata matokeo mazuri wanaelewa kitu ambacho nataka kukufundisha kwenye post hii.

Kitu hicho ni Namna ambavyo mfumo wa Facebook au Instagram wa kufanya matangazo ya kulipia unavyofanya kazi.

Sikiliza, ukijua namna ambavyo mifumo ya matangazo ya Facebook na Instagram inavyofanya kazi inakuwa ni rahisi kwako kujua ni nini ufanye ili uweze kupata matokeo mazuri.

Kwahiyo nataka (kama utaniruhusu) kwenye post hii nikufundishe namna ambavyo mifumo ya kufanya matangazo ya kulipia Facebook na Instagram inavyofanya kazi.

Lakini kabla sijakufundisha nataka nikutolee mfano mmoja ambao utakufanya uelewe darasa hili haraka na kirahisi tu.

Tuchukulie mfano una simu ambayo ina mfumo wa Face ID.Yaani unaweza ukaseti simu yako ijifungue pindi unapoelekezea sura yako kwenye screen.

Kuseti simu yako ijifungue pindi unapotazama kwenye screen lazima kwanza ujipige picha tofauti tofauti ili sura yako itambulike na kumbukumbu za sura yako zitunzwe kwenye mfumo huo...

Ili pindi unapotazama kwenye screen camera ya mbele inachukuwa picha ya sura yako halafu inatuma taarifa kwenye mfumo ili mfumo ufananishe sura hiyo na ulizozihifadhi kuona kama ni wewe.

Baada ya mfumo kujihakikishia kuwa ni wewe ndio screen inafunguka.Mchakato huo unatokea haraka sana kana kwamba hata sekunde moja inaweza isifike.

Sasa jinsi hiyo ambavyo mfumo wa Face ID kwenye simu yako unavyofanya kazi ndivyo hata mfumo wa kufanya matangazo ya kulipia Facebook au Instagram unavyofanya kazi.

Uki-log in kwenye account yako ya Facebook au Instagram Mfumo unafuatilia kila kitu utakachokifanya.Kwa mfano; kama baada ya “kulog in” utaonesha kusoma post au matangazo au chochote kuhusu mpira, Roboti litakuweka kwenye “Kundi la watu wanaopendelea mpira”

Kama tena utaonesha kusoma post au matangazo kuhusu masuala ya afya, Roboti litakuweka kwenye “kundi la watu wanaopendelea masuala ya afya”

Ninachokimaanisha hapa ni kwamba Tabia yoyote ile mpya utakayoionesha uwapo mtandaoni, Roboti litakuweka kwenye “kundi la watu wengi wenye tabia hiyo”

Tabia hizo Facebook au Instagram anaziita “Interests” Kwahiyo interests ni makundi ya watu wenye ufanano wa tabia wawapo huko mtandaoni.

Sasa, unaporusha tangazo lako la kulipia Facebook au Instagram siku 7 za mwanzo mfumo unakuwa kwenye “Learning Phase”

Yaani unafanya majaribio ya tangazo lako kuona ni makundi gani ya watu wana mwitikio mzuri kwenye tangazo lako.


Majaribio haya ni mfano wa jinsi ambavyo camera ya mbele inavyochukua sura yako na kutuma taarifa kwenye mfumo Face ID kwenye simu yako kufananisha sura yako na picha za sura yako ambazo zipo kwenye mfumo tayari ili kuruhusu screen ya simu yako ijifungue.

Kwahiyo baada ya mfumo wa Facebook au Instagram kugundua ufanano wa tabia za watu wenye mwitikio mzuri kwenye tangazo lako, mfumo unatafuta kundi kubwa la watu wenye sifa hizo na kulionesha tangazo lako kwa watu hao na kufanya iwe rahisi kwako kupata matokeo mazuri.

Hiyo ni taarifa njema.Taarifa mbaya ni kwamba majaribio hayo yanafanyika pindi unapokuwa umefanya tangazo la kulipia.

Kwahiyo hela yako ndio inatumika kufanya majaribio hayo.Kwahiyo hii ni taarifa njema kwa wafanyabiashara wakubwa wenye bajeti kubwa kwasababu wao wanaweza wakavumilia siku hizo 7 za majaribio.

Wakati kwa mfanyabiashara mdogo ni kilio na kusaga meno maana kuvumilia bajeti yako itumike kwenye majaribio ni haiwezekani.

Na ikumbukwe kwamba kipindi cha majaribio cha siku 7 (Learning phase) unaweza usipate matokeo yoyote kwasababu Mfumo unakuwa unajaribu kubaini watu ambao wana mwitikio mzuri kwenye tangazo lako...

Ili baada ya majaribio ndio uanze kukupatia matokeo mazuri.Na kama ulikuwa hujui ni kwamba kila uki-edit tangazo hata kama umebadili neno moja kwenye tangazo lako, Kama tangazo lilikuwa lishatoka kwenye kipindi cha majaribio linarudi tena kujaribiwa kwa siku 7 zingine.

Kwahiyo punguza tabia ya kuedit tangazo lako kila iitwayo leo maana utajikuta tangazo lako kila siku lipo kwenye “learning phase” 

Kwanini mfumo unafanya majaribio?

Kwasababu mfumo haumjui mteja wako ni nani lakini kupitia kufanya majaribio ndipo utakapogundua watu wenye mwitikio mzuri kwenye tangazo lako na hivyo.

Kulionesha tangazo lako kwenye kundi kubwa la watu wenye sifa za kufanana na watu wenye mwitikio mzuri kwenye tangazo lako.

Je, kuna njia ya kuzuia upotevu wa hela nyingi wakati mfumo unafanya majaribio?

Ndio, zipo njia 2.

Njia hizo 2 zinafanya kazi ya kuusaidia mfumo uwahi kubaini watu wenye mwitikio mzuri kwenye tangazo lako na hivyo kuzuia majaribio ya siku zote 7 ambazo zingepelekea upotevu wa hela nyingi.

Njia ya kwanza ni kutumia...

“Meta Pixel”

Meta pixel ni maandishi fulani (Code) ambayo kupitia “Business manager” yako unayatengeneza.Halafu baada ya hapo unayakopi kisha unaenda kuyapesti kwenye tovuti (website) yako.

Kazi ya hii meta pixel ni kunukuu kila kitu ambacho mtu atakifanya baada ya kutoka Facebook au Instagram kuja kwenye tovuti yako.

Kwa mfano kama umeseti mtu akiona tangazo lako Facebook au Instagram aje kwenye tovuti yako na akifika kwenye tovuti yako umeweka utaratibu wa mtu huyo kununua bidhaa au huduma yako hapo hapo kwenye tovuti yako.

Kwa kufanya hivyo unausaidia mfumo kubaini hicho ambacho watu wanakifanya wakifika kwenye tovuti yako.

Kwahiyo Mfumo utalionesha tangazo lako kwa watu wengi wenye sifa za kufanana na hizo za watu wanaonunua pindi wanapofika kwenye tovuti yako.

Kwa kutumia hiyo meta pixel unapunguza siku za tangazo lako kuwa kwenye majaribio. Badala ya siku zote 7 unaweza ukajikuta inakuwa ni siku moja au 2 tu.

Hiyo ni taarifa njema, si ndio?

Ndio na hapana.

Ndio kwa mtu mwenye tovuti yake. Hapana kwa mtu asiyekuwa na tovuti yake. Na taarifa mbaya zaidi ni kwamba 99% ya wafanyabiashara wa Tanzania hawana tovuti zao.

Sasa kama huna tovuti utatumia nini kuzuia upotevu wa hela nyingi wakati mfumo unafanya majaribio?Jibu ni rahisi. Unatumia njia ya pili. Njia ya pili ni.

“Targeting Hack”

Targeting hack ni mbinu ya kugundua makundi ya watu ambao wana sifa za ufanano na wateja wako.Makundi hayo ni “Interests” sahihi za wateja wako.

Ukiweza kuyabaini makundi hayo utaweza kuusaidia mfumo kupunguza siku za majaribio kwa namna ifuatayo...Wakati unarusha tangazo lako Facebook au Instagram badala ya kuuachia mfumo ukutafutie mtu mwenye sifa za kuwa mteja wako...

Unauambia mfumo kwamba mteja wako ana sifa fulani kwa kuweka “Interests” hizo ambazo umezibaini kwa kutumia “Targeting Hack”

Kwa kufanya hivyo, mfumo utalionesha tangazo lako kwa watu sahihi moja kwa moja hivyo kujikuta unapata matokeo ya haraka na kwa bajeti ndogo.

Pengine unajiuliza elimu juu ya kutumia “Targeting Hack” utaitoa wapi? Nina taarifa njema kwako.

Nimeandaa darasa kuhusu namna ya kutumia “Targeting Hack” kubaini makundi ya watu ambao wana sifa za kufanana na wateja wako.

What to Learn

In business and tips are here

UFllRXRaZDJpLytvYUpFSzZoL1c3NWRTbkltV2VJeEgwMUo1Y3ZvNEU0bz01