Vitu muhimu unatakiwa kuwa navyo unapoanzisha tovuti ya wakala wa utaliiWatu wengi wana mapungufu ya ufahamu wa uanzishwaji wa tovuti ya wakala wa utalii wanaojulikana kama wakala wa biashara ya utalii (Tour Operator) na wachuuzi wa safari sa utalii (Travel agents) 

Sasa leo nimeona nitoe somo kwa wale ambao hawana ufahamu sahihi wa jinsi ya kuanzisha biashara ya utalii mtandaoni kwa kujua kanuni zake.

Moja kabla ya kuanzisha tovuti ya biashara ya Utalii lazima kwanza ujue mjenzi wa tovuti wako ni nani na je anaelimu gani ya ujenzi wa tovuti (website) na pia uwelewa wake wa tovuti upo vipi

 Kwa wabunifu wa tovuti pamoja na wahandisi hata kama wamehitimu shahada za uhandisi pamoja na ujuzi wa ujenzi wa tovuti ni lazima wawe wame gawanyika katika sehemu fulani katika ujuzi wao sio kwamba pamoja na kuwa wahandisi wa programu za komputa pamoja na kuwa wabunifu wa tovuti basi ndio watakuwa wamekolea katika maeneo yote ya tovuti. (Kwa kifupi ni kama taaluma ya udaktari) Kuna daktari wa macho kuna daktari wa meno na nk.

Kwa mfano kuna maeneo mbalimbali ya biashara za mtandaoni kama biashara za bidhaa au viwandani pia kuna biashara za wamachinga kwa mfano wale wanaoweka bidhaa zao kama kule KUKUU au JIJI letu .

Hizi tovuti huitwa E-commerce, basi sasa huu ni mfano wa nini wewe unatakiwa kujuwa mbunifu wako yeye amebobea wapi kwa mfano unaona kama yekrinaweb.com imejikita katika kuzalisha tovuti za biashara ya utalii hii ni kwa sababu wamejikita katika kufahamu mfumo halisi wa tovuti za aina hii sio kwamba hawawezi aina nyingine hapana hii ni kuhakikisha wateja wake wanapata kitu halisia katika biashara zao za mtandaoni.

Hivyo ni muhimu kujua kampuni ya uhandisi wa programu za computer na wabunifu wake ili kujiridhisha na utendaji wao kusudi lengo lako la biashara mtandaoni litimie vizuri.

Watu wengi wamefanyiwa tovuti ambazo hazikuleta matokeo mazuri kwa sababu walikosea tuu kutazama na kujuwa aina ya wahandisi na wabunifu waliowatumia katika biashara zao hasa za utalii maana ndio tovuti zinazoitajika kwa wingi hapa Tanzania.


Ni muhimu kujuwa soko na biashara yako ya utalii mtandaoni inalenga wapi

Watu wengi na hata wateja niliokutana nao kwa kweli wanaupungufu na ufahamu wa kile wanachotakiwa kufanya wengi hawajui kabisa ni kama wanakurupuka sana katika kufanya biashara kupitia tovuti. 
Embu fikiria mtu ambaye hajui muundo wa  vifurushi vya  Safari za utalii (Tour packages) pamoja na ratiba ya safari (Itinerary ) huyu anataka afanye biashara na mteja wa kutoka Mtandaoni je hapa kwa kweli inakuwa ni kituko sana jambo la muhimu ni lazima watu wajue bidhaa zao wenyewe na sio kumtegemea mbunifu au wahandisi wa tovuti kwa maana wao wamebobea tu katika eneo lao la taaluma ya ubunifu na  uundaji wa tovuti Japo ni wachache wenye upeo wa maswala ya utalii .

Kwa bahati mbaya wabunifu wengi wanaobuni wavuti za biashara ya utalii hawana wazo au muundo wowote kuhusiana na vifurushi vya safari za utalii (Tour Packages) pamoja na ratiba ya safaris (Itinerary) na ndio maana wavuti nyingi zinakuwa ni za kunakilii sehemu moja kwenda nyingine

Hivyo ni muhimu uanze kujifunza kupitia kampuni kubwa jinsi wanavyo fanya biasha za utalii kupitia mtandao kama ALTEZA,A&Kent na And beyond. huko utajifunza mengi kuhusu biashara ya utalii mtandaoni.


Nini unatakiwa kuandaa kwa ajili ya tovuti ili kupeleka kwa mbunifu au mhandizi wa tovuti?

Hapa ni orodha ya vitu muhimu unavyotakiwa kukusanya au kujuwa kuwa uwe navyo kabla ya kuhitaji tovuti kwa ajili ya bishara ya Utalii:
  1. Hakikisha unaufahamu kamili wa soko lako kwa mfano unataka kupata watalii wakifaransa tuu au kispanishi  je au ni wamerekani tuu ukishajuwa kwamba unataka kushuhulika na wapi ndiposa utajuwa ufanye nini na pia kwa kuzingatia lugha zao
  2. Hakikisha unaandaa vifurushi vya kipekee vya safaris kwenye maeneo husika kuhusu bidhaa yako (Tour packages) na ratiba za bidhaa zako za safari kwa eneo husika (Iternerary) Hakikisha unaanda kulingana na muda wa eneo husika na pia kuzingatia utamu na vionjo vya eneo,mandhari ya vifurushi vya safaris hii ikiwemo malazi na huduma muhimu na zile za nyongeza kwa wateja wako.
  3. Hakikisha unaandaa picha anuwai na video zenye kuleta hamsha hamsha na bashasha pindi wateja wako wanapotembelea tovuti yako wasisimuke na picha na video za matukio halisi katika bishara yako.
  4. Hakikisha una maelezo na nia na hari iliyokufanya uanzishe biashara ya utalii je wewe ni nani na nini kilikufanya uanzishe biashara hio na je nini lengo lako la baadae katika mafanikio eleza kusudi wateja wako wapate sababu ya wewe kuanzisha biashara mtandaoni kwa mfano baadae unalenga katika kutoa huduma kwa watu au jamii inayoitaji msaada au hata kuendeleza mambo muhimu  katika jamii yako ikiwemo shule,kulinda mazingira na nk.nb.ikimbukwe wenzetu weupe wanapenda kujitoa katika jamii na kitu kinaitwa uhisani (philanthropy)  hii itahusiana na  ukurasa wa kuhusu kampuni (About us page).
  5. Shirikiana na maeneo ya malazi (Hoteli,Logi,Local Houses) kupata huduma zao kisha uambatanishe kwenye tuvuti yako.
  6. Uwe na watu shirikishi kwa maana ya (TEAM) watendaji wako wawe katika uwiano sawa mwanamke na waume hiki ni muhimu kwa weupe sana.
Mwisho hakikisha haukai mbali na biashara yako pindi tovuti itakapokuwa tayari kwa maan kuanza kuifanyia promotion na kushirikisha jamii mabambali kama huko facebook,twitter,linkedin bila kusahau kwenye maeneo ya kusaidia kuwatangaza  (tour operators na Travel agents) kama kule safaribooking,tour rader,getyourguide na nk.

Imeandaliwa Kithabiti na mbobezi  (Technical Writer) wa maudhui ya safari za utalii 

LUCK MOSHY 0789545040 
Maudhui yanamilikiwa kisheria DMCA


What to Learn

In business and tips are here

UFllRXRaZDJpLytvYUpFSzZoL1c3NWRTbkltV2VJeEgwMUo1Y3ZvNEU0bz01